GET /api/v0.1/hansard/entries/1570937/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1570937,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1570937/?format=api",
    "text_counter": 109,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kisauni, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Rashid Bedzimba",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa kuchangia majibu haya ambayo yametoka kwa Kamati ya Kiidara ya Elimu. Kwanza, nitapongeza sana Kamati hii kwa bidii na juhudi waliyofanya. Swala hili limechukua muda mrefu kujibiwa lakini wamechukua nafasi na jukumu la kumuita Waziri ili wamuulize. Hata mimi niliulizwa kama nilikuwa na nafasi nikae hapo. Kwa hivyo, nimeridhishwa na majibu hayo kwa moyo wangu wote. Lakini, nahimiza Kamati inayoshughulikia maafikiano walichukue kwa haraka na waafikiane ili wale wanaopata shida kule nje wasipate shida tena. Kuna ajira za jeshi na polisi zinazokuja. Lazima wao wahusishwe katika ajira za kiserikali. Kwa hivyo Kamati iharakishe ili iwe wazi na sheria inayoweza kutumika. Wizara isingoje mpaka korti itoe maamuzi kwamba hivyo ni kinyume cha Katiba. Wizara iwe inafikiria iwapo wametoa leseni na kama watoto wanasomeshwa hapo na wizara iwe tayari kuwahudumia hapa. Asante sana, Mhe. Spika wa Muda."
}