GET /api/v0.1/hansard/entries/1581089/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1581089,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1581089/?format=api",
"text_counter": 483,
"type": "speech",
"speaker_name": "Molo, UDA",
"speaker_title": "Hon. Kuria Kimani",
"speaker": null,
"content": " Nashukuru sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipa fursa hii ya kuchangia Ripoti hii iliyoshughulikiwa na Kamati ya Uwekezaji wa Umma kuhusu Huduma kwa Jamii, Usimamizi na Kilimo kuhusu Ripoti ya Ukaguzi wa utendaji ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali inayohusu utoaji wa huduma kwa watu wanaoishi na ulemavu na Baraza la Taifa la Watu walio na Ulemavu. Hii Ripoti inaangazia hesabu za Mwaka wa Fedha wa 2013/2024 – Mwaka wa Fedha wa 2019/2020. Ingawa Kamati hii imefanya juhudi kubwa ya kuhakikisha kuwa imeangazia ripoti zilizowasilishwa kwake na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, bado kuna kipindi kirefu ambacho hesabu za Baraza hili hazijakaguliwa na Kamati. Ripoti hii inakomea Mwaka wa Fedha wa 2019/2020. Kwa hivyo, kuna miaka mitano ya fedha ambayo haijaangaziwa. Sheria ya Tax Procedures Act inasema kuwa rekodi ambazo Mamlaka ya Ushuru ya Kenya (KRA) inaweza kuja kuangalia katika bishara yako ni ya miaka mitano. Kwa hivyo, hili linakiuka sheria zingine ambazo zilipitishwa na Bunge hili. Tunafaa kuipa Baraza la Taifa la Watu walio na Ulemavu kongole kwa kuwa angalau masuala ya walemavu yameanza kuzingatiwa. Kuna walemavu ambao wamesajiliwa na kuna wale ambao wanapokea shilingi elfu mbili kila mwezi. Haya ni mambo ambayo yanafanyika vizuri na tunawapa hongera. Hata hivyo, ukiangalia, kwa mfano, hii leo tunapojadili masuala ya walemavu, tunafanya hivyo bila ya huduma za mkalimani wa lugha ishara ili ujumbe uweze kuwafikia walemavu wasioweza kusikia. Hili linamaanisha kuwa tunazungumza kuhusu masuala ya walemavu ingawa wasio na uwezo wa kusikia hawatajua kuwa tunayazungumza. Lugha tunayotumia kuwasiliana hawataifahamu kwa sababu katika kikao muhimu kama hichi, hatuna mkalimani wa lugha ishara. Mchakato wa kusajili walemavu umezungumziwa vyema na Mhe. Mama Kipepeo. Alizua mambo ya kusisimua kwa sababu Baraza halizingatii mambo yote ya wale watu wanaoishi na ulemavu. Kuna familia nyingi ambazo zinaathirika kutokana na changamoto za walemavu ambao hawajasajiliwa. Kuongeza chumvi kwa kidonda, kuna walemavu ambao wamesajiliwa maradufu. Kwa hivyo, kuna walemavu ambao hawajasajiliwa na kuna wale ambao wamesajiliwa maradufu. Hii sio haki kwa walemavu. Kiwango cha fedha cha alfu mbili ambacho tunawapa walemavu hakiambatani na hali ya sasa ya kiuchumi. Natumai kuwa Kamati ya Bajeti na Uidhinishaji wa Matumizi ya Bunge la Taifa katika bajeti ijayo, litaangazia suala hili na kuhakikisha kuwa limeongeza hela wanazo pewa walemavu ili iwe zaidi ya elfu mbili ili iambatane na hali ya uchumi ilivyo nchini Kenya. Mambo ya ajira na uwakilishaji wa watu wanaoishi na ulemavu bado ipo chini sana Serikalini na katika sekta binafsi. Kwa mfano, hapa Bungeni, wale ambao walichaguliwa kama Wabunge ni wachache sana tofauti na wengine waliochaguliwa kama Wabunge hapa mbeleni. Kwa kuwa Bunge ni sura ya taifa letu la Kenya, idadi ya walemavu Bungeni innaonyesha kuwa walemavu si wengi katika mashirika ya Serikali na katika sekta binafsi. Msaada wa vifaa ambavyo hutolewa haufuati tathmini sahihi za kitalaam. Hii ndio sababu Mwenye Kiti alisema vifaa vingine ambavyo walemavu hupewa vimepitwa na wakati. Vingine ambavyo vinahitaji batteries, unapata wanapewa bila ama zinakuwa hazifikishi mwaka moja kama inavyo stahili. Haya ni mambo ambayo kabisa lazima tuyaangazie kana Bunge ikiwa kabisa tunataka kuwasaidia wale ambao wako na ulemavu. Tungependa Serikali ifanye tathmini mpya ya kiwango cha marupurupu ambacho kinalingana na ugumu wa ulemavu, hali ya uchumi na lengo kuu. Sasa hivi, walemavu wanapata kiasi sawa, ambayo ni Ksh2000. Hili ni jambo ambalo linafaa kuzingatiwa zaidi. Ulemavu huwa tofauti. Mahitaji ambayo yanahitajika na walemavu yanatofautiana kulingana na aina ya ulemavu ilhali wote wanapewa Ksh2000. Wengine ni walemavu kiasi kwamba hawawezi kutembea, wanahitaji pampers na maneno mengine. Tuweze kutumia teknolojia kuweka kiwango cha marupurupu ya walemavu kulingana na kiwango cha ulemavu . Pia tuhakikishi usajili unafanywa kwa njia ya haki. Wasajiliwe na wabadilishiwe vifaa vyao viwe vyo uendelevu, usawa na athari za wanaolengwa. Waswahili walisema “mtu ni utu, The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}