GET /api/v0.1/hansard/entries/1581284/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1581284,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1581284/?format=api",
"text_counter": 62,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kaunti zilipata Shilingi bilioni 375. Kamati ya Fedha na Bajeti imefanya kazi nzuri ili kaunti zipate Shilingi bilioni 28 zaidi. Hii inamaanisha miradi ya maji, barabara, elimu, kilimo na mambo mengine kule mashinani yatafaidika. Gavana wanataka kuwafanyia kazi wananchi inavyofa. Bw. Spika, ningependa kushukuru Kamati ya Mediation kwa ile kazi wamefanya ili tupate hizi hela. Katika Kaunti ya Embu, tulikuwa na Shilingi bilioni 5.3. Pia niko na furaha kwa sababu kaunti 12 zitapata pesa zaidi ya kaunti zingine. Kuna wale walileta hoja ya kuongezea hizi kaunti pesa na walifanya vizuri, nikiwa mmoja wao. Kaunti ya Embu imekuwa na shida ya pending bills na wage bill lakini tutapata Shilingi milioni 600. Kwa hivyo, huu mwaka tunaoanza mwezi wa Julai, tutakua na Shilingi bilioni sita. Bw. Spika, yangu ni kwa Kaunti ya Embu. Tunaomba Gavana Cecily Mutitu Mbarire kwamba hizi pesa zikija mashinani, apunguze madeni, atekeleze miradi ya barabara, maji, kilimo na mambo mengine mengi ili asaidie watu wa Kaunti ya Embu. Pia najua kuna shida ya hela kutoka kwa zile pesa kaunti inakusanya. Ili mwananchi asilie tena na asilete shida, ninaomba Gavana asiongeze ushuru wa kaunti ili wale wamekuwa wakileta shida kama business community wafaidike. Bw. Spika, kuna yale mambo yalifanyika juzi. Nasema pole kwa wale waliopata shida kwa sababu ya maandamano. Tunajua maandamano yanaruhusiwa kikatiba. Pia kwenda kuomboleza kunaruhusiwa kwa sababu kuna democracy . Mambo ya maajabu ni kwamba kuna yale yalifanyika Kaunti ya Embu. Ninasema pole kwa business community. Tuliona ofisi ya Kenya Revenue Authority (KRA), duka la Safaricom, ofisi za National Social Security Fund (NSSF) na National Bank ziliporwa. Pia Maathai Supermarket iliporwa. Ningeomba ikiwa tutakuwa na maandamo siku nyingine kwa sababu ni mambo ya demokrasia, kusitokee mambo kama hayo. Saa zile tunaongezea pesa za kaunti, tunahuzunika sana tukiona watu wakienda maandamano kwa sababu ya haki yao, lakini kunaingia matapeli na wezi na wanaleta vitu ambavyo havifai. Kuna wale walifanya matendo hayo ya uwizi na uporaji wa mali ya wananchi. Bw. Spika, tumeona watu wengi walikuwa wamechukua mikopo na wamepoteza mali yao. Pia kule Embu, vitu viliibiwa kama huku Nairobi. Siku ya Jumatano ilikuwa ya maandamano yanayofaa, lakini baadaye kuligeuka na kuleta shida katika nchi yetu ya Kenya. Watu wengine waliingilia hayo maneno ikawa ni kama wanataka kupindua hii Serikali ambayo inajaribu kulainisha mambo ya economic recovery . Bw. Spika, nawashukuru sana Maseneta kwa ile kazi wanafanya kupigania ugatuzi, ingawa nilisikia Wabunge wengine walipokuwa wakijadili haya maneno, walipinga huu Mswada. Ningeomba magavana wote 47 wasituangushe. Tunawaunga mkono na wafanye kazi vile inavyofaa katika idara zote. Pia kuwe na accountability . Bw. Spika, nikiwa Seneta wa Kaunti ya Embu, niko na furaha kwa sababu Kaunti ya Embu itapata mgao wa Shilingi bilioni sita, kutoka kwa Shilingi bilioni 5.300 kwa sababu tumeongezewa milioni mia sita. Ninataka watu wa Embu wajue kazi itaendelea vizuri na mambo yatakuwa sawa."
}