GET /api/v0.1/hansard/entries/1582560/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1582560,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1582560/?format=api",
"text_counter": 546,
"type": "speech",
"speaker_name": "Msambweni, UDA",
"speaker_title": "Hon. Feisal Bader",
"speaker": null,
"content": " Ahsante sana, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi niongeze sauti kwa mjadala wa Mswada huu muhimu wa marekebisho ya Katiba. Mswada huu ni muhimu sana. Hii ni kwa sababu tukikumbuka shule nyingi za msingi na za upili katika sehemu zetu zilijengwa kupitia harambee na michango midogo midogo ambayo wananchi walijitolea. Nilipojiunga katika shule ya upili, niliweza kutozwa pesa ya kununua basi la shule. Lakini, kwa bahati mbaya ama nzuri, nilisomea katika shule hiyo miaka minne na nilivyo toka baada ya kumaliza Kidato cha Nne, bado basi lilikuwa halijafika shuleni. Lakini leo hii Hazina hiyo imeweza kuwatolea Wakenya mzigo mkubwa waliokuwa nayo. Ni kwa sababu hii walijitokeza kwa wingi kuunga mkono Mswada huu katika public participation . Jambo la pili ni hili: Hazina hii pia imeweza kusaidia watoto wengi kutimiza ndoto zao za kimaisha. Tumeskia ushuhuda kutoka kwa Mhe. Kimani Kuria. Leo tukisema wale watoto wote waliofaulu ama waliosaidika kupitia Hazina ya NG-CDF wajitokeze, basi nina imani wakipiga foleni, wanaweza kutoka hapa mpaka Mombasa na kupindukia. Hazina hii inashughulikia maendeleo katika eneo bunge ambayo ni majukumu ya Serikali kuu pekee kama vile maswala ya elimu, usalama na mazingira. Hazina hii imetolewa katika ule mgao wa Serikali kuu pekee. Kwa hivyo, ninawaambia wale wanaosema kuwa ipelekwe katika serikali za ugatuzi kwamba haitaweza kupelekwa kule kwa sababu inashugulikia maswala yanayohusu Serikali kuu. Ninataka kuwaimiza Waheshimiwa wa Bunge wanaokaa katika Bunge hili kuwa, Jumanne, kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, tujitokeze kwa wingi ili tuhakikishe tunatilia mkazo yale matakwa ya Wakenya ambao The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}