GET /api/v0.1/hansard/entries/1584787/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1584787,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1584787/?format=api",
"text_counter": 287,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika, kwa fursa hii adhimu. Nami pia ni moja wa wanakamati tuliofanya maelewano katika Mswada huu. Kwanza, nachukua fursa hii kuipongeza Kamati andalizi ambayo imefanya mikakati hii. Haikuwa jambo rahisi, na tulikuwa na swintofahamu hapa na pale, lakini mishowe tuliafikiana. Ugatuzi ulikuja ili kufikisha huduma kwa wananchi wa chini. Wajibu wa kamati hii ulikuwa ugavi sawa wa rasilimali baina ya serikali Kuu na serikali za ugatuzi. Kwa sasa, serikali za ugatuzi zimeongezewa fedha katika mgao wao. Naomba tu magavana wahakikishe kuwa huduma zinafikia wananchi, haswa katika sekta ya afya. Utapata mgonjwa anakufa katika Intensive Care Unit (ICU) kwa sababu saa zingine mashine zinazimika ama hazifanfyi kazi. Kama Mama Kaunti, nimejibidiisha kuhakikisha ongezeko katika kaunti ya Mombasa, na kaunti zinginezo. Kwa hivyo, naomba magavana wahakikishe kuwa huduma kama za barabara zimezingatiwa. Kitu ambacho nahitaji kutoka kwa magavana ni kuhakikisha kuwa huduma na vile vile barabara ni bora. Hii ni kwa sababu kutoka shillingi bilioni 405, tumeweza kusukuma hadi tumefika bilioni 415. Zaidi ya hiyo, kunazo shilingi bilioni 55 zimetengwa kwa ujenzi wa barabara. Pia kunazo shilingi bilioni 10 ambazo ni za Equalisation Fund . Ukijumlisha hizi pesa zote katika zile ambazo walikuwa wanataka, shilingi bilioni 450, hata zimeongezeka zimefika kama bilioni 485. Kwa hivyo, kitu ambacho tunataka serikali za kaunti kuhakikisha ni kuwa huduma na madawa yawe yanapatikana hospitalini. Hatutaki kuona mama ambaye amejifungua analipishwa kupokea huduma, na mtoto pia analipishwa. Huo ni wizi au ni dhuluma. Hatutaki kuona wagonjwa hospitalini wanakosa madawa. Juzi na hata jana, tulishuhudia katika mkutano waliokuwa maafisa wa Kenya Medical Supplies Agency (KEMSA) kwamba bilioni 90 imepotea kwa sababu madawa zili expire ilhali Wakenya wanakosa madawa katika hospitali. Mhe.Spika, ukiangalia barabara zinazojengwa Mashinani, unapata zinawekwa patches, vinawekwa vitambara. Barabara hazijengwi vizuri kwa sababu kuna mtu amekaa mahali anajua atajenga barabara vibaya, halafu kesho na kesho kutwa, pesa zingine zitakuja na atazidi kuweka viraka. Mhe. Spika, tumekuwa tukipoteza pesa nyingi sana katika kaunti zetu, na Wakenya wanaangalia. Vijana na kina mama wanaangalia huduma gani inayo kuja mashinani. Na kama alivyosema ndugu yangu, Mhe. Osoro, licha ya kaunti kupata mgao mdogo sana – kama vile Mombasa imetengewa shilingi milioni 46 – tunawawezesha kina mama mpaka watu wa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}