GET /api/v0.1/hansard/entries/1584788/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1584788,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1584788/?format=api",
"text_counter": 288,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": "bodaboda. Juzi mmeona niliwawezesha watu wa bodaboda 40. Vijana wanafurahi na hiyo pesa kidogo. Ukiangalia kina mama, wanapata pesa ya kuwawezesha kufanya biashara. Kaunti wanazo pesa za kuwapatia vijana na akina mama ambayo inaitwa Revolving Fund. Huu ni mwaka wa tatu tukiangalia pesa kukosa kufika Mashinani, na akina mama wanataka kuweka biashara. Wanafanya Serikali ya Taifa hili kulemazwa. Kila wakati, Rais analaumiwa, ilhali kunao viongozi wamepewa nafasi kuweza kufanya kazi, na hawafanyi kazi. Hizi pesa tumewapa, tunataka mjenge Early Childhood Development (ECD) classes. Kuna wengine tuliona hata Seneta alifanya oversight . Alitoa ripoti yake iliyobainisha kuwa shule inaandikwa kuwa imejengwa na shilingi milioni 100, lakini ukiingia ground, hakuna skuli. Nataka kuwaambia magavana kuwa zile kesi nyingi mmetupelekea kule kotini tumekuwa"
}