GET /api/v0.1/hansard/entries/158777/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 158777,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/158777/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Dr. Shaban",
"speaker_title": "The Minister of State for Special Programmes",
"speaker": {
"id": 139,
"legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
"slug": "naomi-shaban"
},
"content": " Ahsante sana, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi hii ili nizungumze juu ya jambo hili ambalo linawakera Wakenya sana. Siku hii ni ya pili. Tumekaa hapa na Bunge hili la Kumi limekuwa ni la wanasarakasi badala ya kufanya kazi iliyotuleta hapa.Tumekuwa tukifanya shughuli ambazo ni za kisiasa badala ya kufanya shughuli za Bunge hili. Bw. Spika, mwaka jana baada ya uchaguzi, Wakenya waliteseka sana! Wakenya walifurushwa makwao; Wakenya wameuana na Wakenya wengine wamebaki kiholela- holela, hawajui kama wao ni Wakenya au sio Wakenya! Bw. Spika, wakati huo huo, Wakenya walitulazimisha kukaa kwenye meza moja ili tuwe na Serikali ya mseto. Sasa hivi, Serikali ipo lakini kazi ambazo tunatakikana kuzifanya, tumesahau kuzifanya. Badala yake, tumeamua kufanya biashara kichaa kuwadanganya Wakenya badala ya kufanya kazi! Kila kukicha, Bw. Spika, wakati tunatakikana kutengeneza kamati hii ambayo itaendesha shughuli za Bunge, tumeamua kuwa kila mtu anataka kuligawia kiwango cha shughuli hii, ama ile ama ile nyingine! Na kila mtu yuko tayari kuja hapa kuweza kuzungumza lake na kusoma Katiba kiasi ya vile ambavyo amejaribu kuielewa ama kujifurahisha; yeye na huyo mkubwa wake ambaye amemtuma! Bw. Speaker, nafikiria kuwa kwenye Katiba, ni wazi kwamba tuna Raisi mmoja na Waziri Mkuu mmoja na, vile vile, tuna Makamu wa Raisi mmoja. Tunaomba kwamba, wakati huu ambapo Bunge la Kumi liko kazini kwa Muhula huu wake wa Tatu--- Muhula wa Kwanza na wa Pili, hatukusikia kukuru kakara hizi! Lakini, sasa hivi, tumeamka na tulikuwa ndotoni na tumegundua kuwa anayetakikana kusimamia shughuli hizi za Bunge hawezi kuwa ni yule yule! Bw. Spika, naomba utuonyeshe njia moja kwa moja! Ahsante sana, Bw. Spika."
}