GET /api/v0.1/hansard/entries/1588731/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1588731,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588731/?format=api",
    "text_counter": 130,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi North, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Mhe. Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi kuunga hoja ya makubaliano ya Bunge kuhusu Mswada huu. Niseme kwamba huu ni Mswada muhimu sana. Ninampongeza Mhe. Ruweida Mohamed kwa kujali watu wake wa Lamu na Pwani. Hawa wanyama tunaowaweka katika ratiba ya wale ambao wakiumiza watu watalipwa fidia ni viumbe walioko baharini. Viumbe hawa wamekuwa wakiwadhuru sana watu wa Lamu, kwani wengi wao hupata chakula chao cha kila siku kupitia Bahari ya Hindi."
}