GET /api/v0.1/hansard/entries/1588760/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1588760,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588760/?format=api",
"text_counter": 159,
"type": "speech",
"speaker_name": "Nakuru Town East, UDA",
"speaker_title": "Hon. David Gikaria",
"speaker": null,
"content": " Asante, Mhe. Spika wa Muda. Ninamshukuru Mhe. Ruweida Mohamed kwa kuwasilisha Mswada huu Bungeni, ambao unalenga kuwajali watu wa maeneo ya Pwani, ambako kuna bahari, na ambapo watu hupoteza maisha au hujeruhiwa kutokana na wanyama walioko baharini. Hili ni jambo muhimu sana kuliangazia. Kuna wakati nilijaribu kuleta Mswada hapa Bungeni kwa sababu kule kwangu, watu wengi hujeruhiwa n ahata kufariki kutokana na mashambulizi ya nyani. Nilijaribu kupendekeza kwamba nyani waorodheshwe kama wanyama wa porini ili waathiriwa waweze kulipwa fidia, lakini haikuwezekana. Namshukuru sana Mhe. Ruweida Mohamed kwa Mswada huu. Natumai kwamba hata sisi, siku za baadaye, tutaangaliwa kwa sababu ya nyani ambao wanasababisha madhara mengi sana katika miji mikuu, hasa iliyo karibu na Hifadhi ya Taifa ya Nakuru, ambapo watu wengi huathirika. Kwa hivyo, niseme kwa mara nyingine tena, pongezi Mhe. Ruweida Mohamed kwa kuwasilisha Mswada huu Asante, Mhe. Spika wa Muda. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}