GET /api/v0.1/hansard/entries/1588765/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1588765,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588765/?format=api",
    "text_counter": 164,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Lamu East, JP",
    "speaker_title": "Hon. Ruweida Mohamed",
    "speaker": null,
    "content": " Mhe. Spika wa Muda, naomba kutoa hoja kwamba Mswada wa Hifadhi na Usimamizi wa Wanyama Pori (Marekebisho) (Mswada wa Bunge wa la Kitaifa, nambari tatu wa mwaka elfu mbili ishiri na tatu), sasa usomwe mara ya Tatu. Pia, naomba Mhe. Owen Baya kuafiki Mswada huu. Nachukua nafasi hii kuwashukuru Wabunge wenzangu kwa kuungana pamoja na kupitisha Mswada huu. Pia nashukuru uongozi wa Bunge kwa kuhakikisha kwamba hivi leo tumefika hiki kipindi cha Kusomwa Mara ya Tatu. Hili ni jambo kubwa sana kwetu kwa sababu tuliona madhara mengi wakati Kamati ilipoenda Faza, kama vile, watu walikuwa wamekatwa miguu. Sasa hivi, kila mwezi lazima angalau mtu mmoja atakuwa amepigwa na huu mnyama anayeitwa Nyenga, kwa kizungu Stingray . Pia kuna watu wengi walioathiriwa. Hii itasaidia watu wetu na pia watalii. Kuna mtalii alienda kupigia picha kisha akaumwa na papa. Pale ferry, watu wengi wanaathirika na papa kwa sabu meli zikija zinapita na papa, ikiwa pengine bahati mbaya mtu ameingia chini ya ferry kutengeneza, anaumwa na papa na hawapati malipo. Mswada huu utasaidia hata hawa Wabunge wanapoenda kujivinjari kule Mombasa wakienda na zile boti bahati mbaya ukianguka kwa maji au ukiogelea, mara nyingine hatari yaweza tokea, pia hao watakuwa wamesaidika. Sitaki kuchukua muda mwingi zaidi lakin nashukuru sana hata nimeshikwa na shaki. Kwangu hili ni jambo kubwa sana. Watu wa Pwani sasa watajihisi kwamba ni Wakenya na wao hawatengwi kwa sheria, kwa maana sheria mwanzo ilikuwa imenufaisha watu kwa ardhi wala sio sisi ambao tunazingirwa na maji ilikuwa hatuonekani. Bunge hili sasa limefanya kwamba watu wanaokaa kwa visiwa vya bahari ama mazingira ya maji, nao pia wamewekwa kwa mpangilio wa serikali. Mara mingi walikuwa wameona kwamba wametengwa. Hii itafanya tuweze kuhifadhi zaidi wanyama wetu wa pori. Ahsante sana, nisije nikalia."
}