GET /api/v0.1/hansard/entries/1588767/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1588767,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1588767/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Kilifi North, UDA",
    "speaker_title": "Hon. Owen Baya",
    "speaker": null,
    "content": " Ahsante sana Mhe. Spika wa Muda. Naafiki Mswada huu uweze Kusomwa kwa Mara ya Tatu. Kama vile Wabunge wenzangu na Mhe. Ruweida walivyosema, huu ni Mswada nzuri sana ambao utasaidia watu wa pwani. Kilifi ni kati ya zile kaunti zilizona ufuo wa bahari mrefu sana na watu wengi kazi yao ni ya ubaharia. Mswada huu umekuja kwa wakati wake ambapo watu wengi waliokuwa wamesahaulika katika maneno ya kufidiwa katika zile ajali zinazofanyika ndani ya bahari sasa pia wamepata nafasi. Naomba uongozi wa Bunge kwamba Mswada huu upelekwe kwa haraka sana ili iwekwe sahihi na Rais, ili usikae. Nimeona Miswada mengine tumepitisha hapa imekaa sana bila kupelekwa kutiwa sahihi. Mswada huu ambao Mhe. Ruweida ameufanyia kazi sana na kuweka matumaini kwa watu wa Lamu na Pwani, ufikishwe kwa haraka sana kwa Rais ili aweke sahihi iliwanaoumia kwa sababu ya hii maneno inayofanyika wapate fidia kwa haraka. Naunga mkono. Ahsante sana."
}