GET /api/v0.1/hansard/entries/1589128/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1589128,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589128/?format=api",
    "text_counter": 169,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "The Senate Minority Leader",
    "speaker": null,
    "content": " Asante mstahiki Spika. Kwanza najua tuko katika hali ya panda kwa sababu mashtaka yaliyoko mbele yetu ni mazito. Hii ni kazi mojawapo ambayo lazima Maseneta waifanye. Ni jukumu langu kuunga mkono yote aliyoyasema Kiongozi wa Walio Wengi kwamba Hoja iliyopo hapa ni ya kumng’atua gavana kutoka kwa mamlaka. Hata hivyo, hivi sasa tunajadiliana kama tutaendelea ama hatutaendelea na hii kesi kwa sababu ya yale yaliopo mbele yetu. Kwanza, ningependa kufahamisha Maseneta wenzangu kwamba mashtaka yalio mbele yetu yana uzito sana. Ikiwa yatadhihirishwa kuwa kweli, basi hatua itakayochukuliwa ni kukubaliana na ile preliminary objections iliyopo hapa ama kuikataa. Kuna uzito wa aina yake. Kwa hivyo, katika uamuzi wetu, tunafaa tupime na kuchunguza iwapo kweli kuna shida ndani ya Kaunti ya Isiolo. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}