GET /api/v0.1/hansard/entries/1589131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1589131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589131/?format=api",
"text_counter": 172,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Madzayo",
"speaker_title": "The Senate Minority Leader",
"speaker": null,
"content": "tujue ya kwamba tutakuwa tumechukua hatua ya juu sana. Vile vile ikiwa tutaachilia, tutakuwa tumechukua hatua ya juu. Hii ni kwa sababu tunajua vile mashtaka huwa kwamba Gavana aking’atuliwa kwenye mamlaka, huwa hana mbele wala nyuma kwa kuenda au kufanya chochote. Atakuwa hana haki ya kushika kazi ndani ya ofisi ama kupewa kazi yoyote. Ni jukumu letu sisi kuangalia kama mashtaka haya yana haki ya kuendelea mbele kulingana na zile stakabadhi ambazo tuko nazo au la. Naona huu ni mtihani mkubwa sana kwa Bunge la Seneti. Lakini niko na imani na hili Bunge la Seneti. Wengi wetu hapa ni mawakili, wafanyibiashara na watu waliobobea katika nyanja mbalimbali. Tuko na magavana wazamani ambao wameweza kutoka katika kaunti zao na wako hapa ndani. Wataweza kutueleza katika ujuzi waliyokuwa nao. Mimi naona hili ni jambo ambalo sisi sote lazima tulizingatie. Bw. Spika, ikiwa nitasimama hapa na kuunga mkono Kiongozi wa Walio Wengi kwa Hoja hii ni kwamba sote, nyoyo zetu tuziweke wazi, tuangalie hii kesi kikamilifu na tuwe na uwezo wa kuamua ili haki itendeke. Niko na imani vile Wakenya wote wako na imani na Bunge la Seneti. Leo ni mtihani mkubwa sana kuona ya kwamba sisi tutasimamia haki kuona kwamba kama ni udhaifu ambao umeletewa gavana, basi tunaweza kusimamisha. Pia kama ni udhaifu umeletewa watu wa Kaunti ya Isiolo, tunaweza kusimamisha. Tutatenda haki kulinganisha na vile tulivyoinua Katiba na tukasema tutalinda Katiba kama kiongozi wa nchi yetu. Asante, Bw. Spika. Naunga mkono Hoja hii."
}