GET /api/v0.1/hansard/entries/1589166/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1589166,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589166/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa hii nafasi. Hapo awali kabla sijakuwa Seneta, nilikuwa mwakilishi wadi katika Gatuzi ya Kirinyaga. Zaidi, nilikuwa Kiongozi wa Wengi. Wakati huo huo, tuling’atua gavana, tukamleta hapa na akarudi, na ni sawa, bado pia yuko. Kuna umuhimu kwa kikao cha bunge la gatuzi kukaa mahali ambapo panajulikana na pamewekwa kwa gazeti la Serikali. Ninakumbuka wakati huo, vichwa vyetu vilikuwa vinatakikana lakini, sisi zote tuliokuwa tumeamini na kuamua ni lazima gavana aende, tulilala katika Bunge la Gatuzi la Kirinyaga ili kuhakikisha tumefanya kazi yetu. Ni kwa nini? Ili kufuata sheria na kanuni zilizowekwa. Kwa hivyo, uhitaji wetu kama Seneti ni kufanya jambo lililo halali na sheria. Chumvi haina maana kwa mtu anayekunywa chai. Vile vile, sukari haina maana kwa mtu anayekunywa supu. Sisi tutakuwa hatuna maana kama tutafanya uamuzi ambao unakizana na sheria za nchi hii."
}