GET /api/v0.1/hansard/entries/1589249/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1589249,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589249/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": ", ama itapatikana wakati itasikilizwa mpaka mwisho? Seneti ikifanya makosa kumbandua gavana mamlakani, huyo gavana ana nafasi ya kuenda Mahakama ya Juu au High Court, Mahakama ya Rufaa na hata Mahakama ya Upeo zaidi katika nchini yetu. Hapa hatuamui kama tunambandua gavana ama hatumbandui. Kile tunachoamua ni kama tutasikiza ushahidi wote kamili ili tuweze kupata taswira ya yale ambayo yalitokea kule Isiolo. Kama ushahidi ambayo utasikizwa hautaweza kufikia kile kiwango kinachohitajika na sheria, basi itakuwa hatuna budi ya kumuachilia. Kwa sasa, itakuwa ni kinyume na dhulma kwa watu wa Isiolo iwapo tutaweza kumaliza kesi hii katika mahali ambapo imefikia ambayo ni hatua ya mwanzo kulingana na sheria. Ninapinga hoja ya kupitishwa kwa hii preliminary objection . Tuache kesi iendelee mpaka mwisho kwa sababu hakuna kile ambacho tutapunguza ama kuongeza tukienda mpaka mwisho."
}