GET /api/v0.1/hansard/entries/1589272/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1589272,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589272/?format=api",
    "text_counter": 313,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii. Kwanza kabisa, swali ambalo tunapaswa kujiuliza pingamizi hii ya awali inaletwa kwa nini? Ni vizuri kwa sababu, katika Seneti hii na vile vile katika gatuzi zetu, tunapaswa kufuata sheria. Ni kinaya ikiwa tunatunga sheria, lakini hatuzifuati sheria zenyewe. Ukiangalia katika Taarifa Rasmi ya Bunge la Isiolo, hakuna kikao chochote kilichofanyika. Kwa hivyo, ikiwa hakukuwa na kikao chochote, sioni kwa nini tunapaswa kushughulikia jambo hili. Ikiwa hapakuwa na kikao chochote na hapo ndipo kungeshughulikiwa mambo haya, Seneti hii inapaswa kusema kwamba hilo pingamizi la awali tunalikubalia ndiposa sheria zifuatwe. Utaratibu wa sheria usipofuatwa, basi hakuna jambo ambalo tutalifanya hapa. Nilimsikia Sen. Faki akisema ya kwamba tuendelee kusikiliza ushahidi wa kutosha ndio tunaweza tukapata mambo mengi zaidi. Ikiwa sheria haikufuatwa kuanzia mwanzo, sioni haja yoyote ya sisi kusikiliza kesi hii kwa sababu, wahenga wanasema kwamba “Usikate kanzu kabla ya mtoto kuzaliwa.” Sisi hatuwezi kusikiliza. Tunajua ya kwamba katika gatuzi nyingi kuna shida nyingi. Laikipia, Nandi, Isiolo na kaunti nyingi kuna shida. Hata hivyo, hatutatua shida bila kufuata utaratibu wa sheria. Ni kinaya kwa sababu sisi ndio tunatunga sheria. Gatuzi hiyo ya Isiolo wanatunga sheria. Ikiwa hatutaweza kufuata Kanuni za Kudumu ambazo sisi tumeziweka, hakuna haja ya kuketi hapa; tunapaswa kuwa tumefunga virago na kuenda nyumbani. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}