GET /api/v0.1/hansard/entries/1589304/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1589304,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589304/?format=api",
    "text_counter": 345,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Wafula",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "vilikuwepo. Jambo la muhimu ni kwamba, je vilikuwa vikao halisi ama gushi? Iwapo vilikuwa vikao halisi, ni lazima wajieleze. Jambo la pili ni video ambayo nimeona iliyoonyesha ofisi iliyovunjwa na vifaa kuharibiwa. Imenipa taswira ya maandamano yaliyokuwepo juzi kwamba Isiolo kuna wahuni na majambazi. Iwapo ni hivyo, lazima tuwafuate na wakamatwe kwa sababu wanahujumu shughuli za Kaunti ya Isiolo. Mwisho, waswahili husema kuku akijipata kwenye kesi ambayo mwewe ndiye hakimu, atapata haki? Iwapo umewafuga kuku na wamevuka ua, na unaona mbweha anawaandama kuku wako, utamfurusha mbweha ama umukung’ute na fimbo halafu umkamate kuku umrudishe kwenye boma? Asante sana, Mhe. Spika."
}