GET /api/v0.1/hansard/entries/1589332/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1589332,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589332/?format=api",
"text_counter": 373,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Miraj",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, kulingana na gumzo ambalo linaendelea, ni dhahiri shahiri ya kwamba kuna hitilafu katika kutimuliwa kwa Gavana wa Isiolo. Nikiunga mkono kauli za wengi ambao wameweza kuzungumza katika Seneti hii, niweze kuzungumza kinaga ubaga ya kwamba ni dhahiri shahiri pia kuwa Wawakilishi Wadi wa Bunge la Isiolo wako na ari na ushahidi wa kutosha kuonyesha kwamba katika gatuzi la Isiolo, kuna matatizo ambayo yanahitaji Bunge la Seneti kuweza kuwasaidia kuyatatua. Hayo ndio majukumu tuliyotwikwa na Katiba yetu ya Kenya, ni vyema wasitumie njia za mkato kumtimua Gavana aliyechaguliwa na wananchi wa Isiolo."
}