GET /api/v0.1/hansard/entries/1589336/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1589336,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1589336/?format=api",
    "text_counter": 377,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa nafasi ya kuchangia mjadala wa kutimua Gavana wa Isiolo. Si vizuri sana kwa sababu kuna mipangilio pale mwanzo Wawakilishi wa Wadi wangepanga ili wawe na kikao kwa bunge la kaunti. Haionyeshi vizuri vile walikaa kwa sababu, katika sheria, kuna pahali wangekaa. Kwa miaka mingi wakati wawakilishi wadi na councillors wakitaka kutimua yeyote, walikua wanaenda wanajificha mahali, lakini hakuna mahali hayo yalikua yanazungumziwa. Lakini, siku ya mwisho ya kikao, hata kama kuna vita vya mishale au bunduki, ni mpaka wangeingia kwa kile kikao ili kuonekana wanafanya kazi gani. Ninaunga mkono Gavana arudishwe kwa sababu, kuna mambo hayajafuatiliwa. Ningetaka kumwambia rafiki yangu, Sen. Eddy, kwamba haimaanishi hatujafuata njia ile inafaa. Kwa Bibilia na Quran, kuna mtu mmoja alijenga nyumba kwa mawe na mwingine akajenga kwa mchanga na wakati mvua ilinyesha, ile nyumba ya mchanga ilianguka. Kwa hivyo, wacha hii nyumba ya Wawakilishi Wadi wa Isiolo iteremke ili iwe funzo kwa kaunti zote 47 ndio wawe na mwanzo wa kufatilia sheria ya kutimua magavana. Ningependa kujibu Kiongozi wa Wengi, Sen. Cheruiyot, kwa mambo yale amesema kwamba kuna tofauti ya Kericho na Isiolo. Ningependa kumueleza kwamba hakuna totafauti kwa sababu ile haikua na mmoja na ikatemwa mbali. Hii naye kutoka mwanzo, hakuna pahali inaonyesha vile wangetimua yule Gavana. Ningependa kujibu Sen. Joyce aliyesema tunatupa wakati. Seneti saa hizi haijatupa wakati sababu tuko Maseneta 67 na tunataka kuonyesha nchi ya Kenya na wanaotuangalia kwamba tuko na ukweli wa kuchambua mambo ya Seneti na watu wengine wakitimua gavana, watafuata njia ile inafaa. Bw. Spika wa Muda, nikimalizia, ninasema turudishe Gavana. Tumejua mambo mengi lakini tunamuomba Gavana akirudi pale - Bibilia inaseme watu wawili hawawezi kutembea bila kuelewana - akae chini na Wawakilishi Wadi, waelewane ndio kaunti ya Isiolo iendelee vizuri. Kwa Wawakilishi Wadi, kama Gavana hataenda wakae kikao kimoja ili kubadilisha Isiolo, tungewaomba wamrudishe na tutamtimua kama watafata ile njia inafaa."
}