GET /api/v0.1/hansard/entries/1592301/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1592301,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1592301/?format=api",
    "text_counter": 658,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Sheria hii inalenga hao watoto ili waweze kupata elimu kama wengine.itawawezesha kuingia shule za kwanza, za upili hadi university . Inalenga elimu yao iwe bure. Hili ni jambo la kutia moyo sana. Pia, katika shule wanaosomea, Serikali ihakikishe wamepata vifaa maalum vya kutumia ili waweze kupata elimu vizuri. Mara nyingi, wanakosa vifaa maalum vya kuwafanya waelewe lile jambo wanalofanya. Ni jambo la kutia moyo sana endapo sheria hii itapitishwa na Bunge hili. Watoto wetu watasoma. Hivi karibuni, nilikumbana na visa dhidi ya watoto walemavu. Wengine wamefungiwa ndani mwa majumba, wengine wanafungwa minyororo wasionekane na jamii. Kama Serikali, tutadhibiti ili tuwe na sheria maalum ya watoto hao kupata elimu nzuri. Kila mzazi atajitokeza kuhakikisha mtoto wake amepata elimu bora na sio bora elimu. Jambo hilo limevunja moyo wazazi wengi kule mashinani. Wanaona watoto wenye ulemavu kama laana fulani kutoka kwa jamii. Lakini sio laana, ni uwezo maalum. Sisi waislamu tunaamini ni maumbile na uwezo wa Mwenyezi Mungu. Yule aliyekutoa wewe mzima, ndiye aliyemtoa yule akawa na mapungufu kiasi. Hatutaki kusema ni mapungufu kwa sababu ni mpango wa Mwenyezi Mungu."
}