GET /api/v0.1/hansard/entries/1604135/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604135,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604135/?format=api",
    "text_counter": 90,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Mstahiki Spika, kwa kunipa nafisi hii ili niweze kuzungumzia jambo la kusikitisha kuhusu kijana Albert Ojwang’. Hata kama Wakenya ni vikaragosi, hakuna vile tutaambiwa ya kwamba yule kijana alikuja kujipigisha kichwa kwa ukuta hapa Nairobi. Kwani wanataka kusema ya kwamba hakuna ukuta kule Homa Bay? Kivuli cha fimbo hakiwezi kuficha mtu jua. Kwa hivyo, hata wakijaribu kuficha jambo hili, bado litatokea wazi. Juzi, maofisa wakuu katika idara ya polisi walisema ya kwamba wale wadogo wao ndio walifanya hicho kitendo. Samaki wote hunuka lakini walimshuku kambare. Kama kuna harufu ama muozo, basi, tutaangalia idara nzima ya polisi, kuanzia juu mpaka chini. Hawawezi kusema ya kwamba ni wale wadogo ndio walifanya kitendo hicho. Ingekuwa ni bwenyenye ambaye ameuawa, watu wangekuwa wamekamatwa. Kuna msemo wa Kiswahili ambao unasema mkata hendi mkele na angenda mkele, The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}