GET /api/v0.1/hansard/entries/1604136/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604136,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604136/?format=api",
"text_counter": 91,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "akipakia jahazi mtele tele hurudi na upele. Hatua ambayo huchukuliwa wakati wakubwa wameuawa ndio pia inafaa kuchukuliwa wakati huu kijana huyu ameuawa. Ukiona kesi inakaa sana katika kasiri ya mfalme, jua ya kwamba tajiri ana makosa. Hii kesi ya huyu kijana imezungushwa. Hiyo ni ishara ya kwamba kuna wadosi fulani ambao wako na makosa. Tusifanye jambo hili liwe la kisiasa. Ukiona kivuli cha mtu mfupi kimeanza kuwa kirefu, jua ya kwamba kunakucha ama ni machweo. Siku moja, machweo itakuja kutufikia. Ninaomba Serikali na taasisi za usalama kuhakikisha ya kwamba wamevalia junga swala hili. Wahakikishe ya kwamba kifo cha Ojwang’ kisiwe tu mtu mwingine amepotea na hakuna kitu kimefanyika."
}