GET /api/v0.1/hansard/entries/1604156/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604156,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604156/?format=api",
    "text_counter": 111,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Mwaruma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika, ninakumbuka wakati wa miaka ya tisini ilikuwa ukiongea unaangalia nyuma na hata ukiwa ndani ya nyumba unasema kuta zina masikio. Kila mahali kulikuwa na majasusi. Hatutaki kurudi maeneo hayo. Ni lazima uchunguzi ufanywe vizuri. Nilileta taarifa katika Seneti ambayo haijapata suluhisho. Ilihusu mtu aliyeuawa kule kwetu Weruga ndani ya mikono ya polisi alikiwa seli. Mwangoji wa Meliza aliuawa na mpaka wakati huu, kamati husika haijaleta ripoti kamili. Ningependa kushinikisha kwamba ripoti hiyo iletwe ili tujue Mwangoji alifanya makosa gani na ni kitendo gani kilifanywa na wale polisi ili afe katika mikono yao. Bw. Spika, ni lazima suala hili liangaliwe kwa undani. Wakenya wasinyamaze wakati kuna mambo ya kashfa kwa sababu ni haki yao kuongea na baada ya kuongea walindwe. Sio kusema kuwa mtu akiongea ukweli huna haki ya kulindwa. Ni lazima tujue tuna katiba inayolinda kila Mkenya. Kulikuwa na uwezekano wa Mwalimu Albert kupelekwa kortini na kufunguliwa mashtaka lakini sio kumwua ndani ya seli."
}