GET /api/v0.1/hansard/entries/1604168/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604168,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604168/?format=api",
    "text_counter": 123,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Chute",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Leo ukiliendesha gari, na ukikimbishwa na wakora, mahali utakimbilia kwanza uokoe maisha yako ni police station . Sasa, ukienda police station ya Kenya na utauawa, ukikimbizwa na wezi, utaenda wapi? Huna mahali pa kwenda kwa sababu mahali unakimbilia na mahali unaenda pia kuna kifo. Hayo ndiyo maisha tuliyo nayo. Askari walioko Kenya ni 108,000 - askari polisi na askari wa Utawala. Nikisimama hapa, nikiwakilisha Marsabit, sitaki kuwalaumu polisi wote. Siku tano zilizopita, mahali panaitwa Loiyangalani, Lake Turkana, Marsabit County, watu wanne waliuawa. Napeana pole kwa familia hiyo. Kama polisi wanaoitwa QRU - QuickResponse Unit – hawangefika huko, saa hizi watu karibu 100 wangekuwa wamekufa. Nawapongeza polisi hao vile walifanya kazi hapo. Mwaka wa 1990 – leo Gavana Orengo alikuja mbele yetu – alikuwa juu ya Toyota Stout akipigania Constitution mpya. Kama angeuawa siku hiyo, hatungepata hiyo"
}