GET /api/v0.1/hansard/entries/1604196/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604196,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604196/?format=api",
"text_counter": 151,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kavindu Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante, Bw. Spika, kwa kunipa fursa hii ili niweze kuongeza sauti yangu kwa hili jambo ambalo linahuzunisha sana. Kwanza, ningependa kuwaambia wazazi wa huyu kijana, pole. Kila mzazi hutarajia kuzikwa na mtoto wake. Hakuna mzazi hata mmoja hutarajia kuzika mtoto wake. Hili jambo linaleta uchungu sana kuona watoto wetu wanauawa kama ndege. Ikifika tarehe ishirini na tano mwezi huu, tutakuwa tumefikisha mwaka tukikumbuka Gen Z wetu walivyouawa. Nilikuwa kwa hili Bunge na nilitoka pale nje tukaenda kule Bunge Tower. Tulikaa masaa matatu kule Bunge Tower lakini ilikuwa kama mwaka mzima. Nikiwa huko wakati nilipokuwa nasikia bunduki ikilipuliwa “tu!” nilikuwa nasikia kama tumbo yangu inatoka kwa sababu mimi ni mama na hiyo bunduki ilikuwa inapiga mtoto. Hivi sasa, tunaongea kuhusu mtoto ambaye ameuwawa na watu ambao wanastahili kuwa wanalinda kila mwananchi katika taifa hili. Kama tutauliwa kule tunastahili kukimbilia usalama, basi, tutapata usalama wapi Kenya hii? Hii ni kuonyesha kwamba taifa letu limeanguka kabisa. Ninaita President wa hii taifa, Bw. William Samoei Ruto, tafadhali, simama kama President sasa hivi, kama sio jana, na uongee kuhusu huyu kijana. Wale ambao wamesababisha hicho kifo chake, watendewe kile wanastahili kutendewa kwa sababu hatutanyamaza watoto wetu wakiendelea kuuawa. Wakifa wote, tutabaki na akina nani kama taifa? Vijana ndio wenye nguvu ya kuweza kuendelesha taifa. Tukizidi kuwauwa, tutapata wapi wengine wa kuendelesha taifa hili? Kama mtu yoyote amefanya makosa, kuna mahakama. Apelekwe mahakama na ahukumiwe. Kama nikufungwa, afungwe. Kama hakuna hatia, aachiliwe. Ninakashifu hili jambo la kuuawa kwa sababu hakuna haki wakati mtu anapoteza uhai wake bila sababu yoyote na ndio mtoto wa pekee wa wazazi wake. Hao wazazi hata labda umri wao hauwaruhusu kuwa na mtoto mwingine. Watapata mtoto mwingine wapi? Hata kama watalipwa fidia, hiyo fidia hailinganishwi na huyo mtoto. Tunaomba haki itendeke hata kwa wale Gen Z waliokufa katika taifa hili."
}