GET /api/v0.1/hansard/entries/1604198/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604198,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604198/?format=api",
    "text_counter": 153,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Okenyuri",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "vijana wa taifa watatendewa unyama kama ule, sisi viongozi tunabaki hapa tukinung’unika, hii sio hali ya kawaida. Mauaji ya wanablogi yamekithiri. Sisi kama viongozi tumezoea kuwekewa makosa kwenye mitandao lakini hatujawahi kuwa na hasira kiwango cha kutaka kuwaua wale wanaotutusi pale kwenye mitandao. Kwa sababu tuko kwenye nafasi za uongozi, mambo kama yale yakitokea, hatupaswi kuchukua hatua kama zile. Kwa hivyo, maafisa wale ambao walimchukua kijana huyu Albert kutoka nyumbani kwao akiwa salama washtakiwe kwa makosa ya mauaji ili waweze kuliambia Bunge hili na taifa kiini kikuu cha wao, na ni nani ambaye aliwatuma kumwangamiza kijana huyu. Roho yake isilale pema peponi. Iweze kuwasumbua wale ambao wamefanya mambo hayo katika taifa hili. Asante sana."
}