GET /api/v0.1/hansard/entries/1604211/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604211,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604211/?format=api",
    "text_counter": 166,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Ojwang’. Ninampongeza pia Seneta wa Migori kwa kuleta Kauli hii. Wakati huu, nchi nzima kuna tanzia kwa sababu ya kumpoteza kijana barubaru, kijana aliyekuwa na maono. Hii imekuwa ni kama kawaida kwa sababu inaonekana watu wanaongea na polisi – maafisa wa usalama wamezoea kuwa watu wataongea na watanyamaza. Ninasema hivyo kwa sababu, kuna kauli ile tungetaka kujua wale waliua Padre John Maina Ndegwa Waboiman. Vile vile, kuna Kauli kuhusu Padre Allois Cheruiyot Bett. Ikiwa huwezi ukapata kauli kama hizi, wanajua ya kwamba, hata huyu kijana tunaeambiwa na maafisa watafanya uchunguzi, hatutapata. Uchunguzi wa kwanza walisema, huko ndani ya seli, Ojwang’ alijigongesha kwa ukuta. Huyu Ojwang’ hakuna mahali panasemekana alikuwa na ugonjwa wa kifafa ama kuanguka. Ni wazi ijulikane kwamba, alipochukuliwa kutoka Homa Bay, maafisa wa usalama walihakikishia wazazi wake kwamba, alikuwa sawa sawa na atapatikana akiwa vile vile. Bw. Spika, alitoka huko akiwa buheri wa afya lakini ukiangalia ripoti ya upasuaji wa mwili wake, inaonyeshana ya kwamba alinyongwa na alipigwa kichapo cha mbwa kuingia msikitini. Hii ni aibu kwa maafisa wa usalama kwa sababu, hao ndio wamepewa jukumu la kulinda mali na maisha ya wananchi. Sasa inafika mahali wananchi wanashindwa wakimbilie majambazi, hapana. Wakimbilie polisi, hapana. Bw. Spika, Inspekta Generali wa Polisi anapaswa kuitwa hapa aelezee kinaga ubaga. Naye naibu wa Inspeka Generali wa Polisi anayetuhumiwa ya kwamba haya mambo yametendeka kwake, anapaswa kuwa amejiuzulu. Si yeye peke yake. Samaki huanza kuoza kutoka kwa kichwa. Waziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, akija hapa kesho anapaswa kutueleza vizuri na akishindwa, ajiuzulu kwa sababu, yeye ndiye tunategemea na yeye ndiye amepewa hilo jukumu kama Waziri. Ningependa kushukuru vijana wa hapa, Seneta Eddy na Kiogozi wa Wengi ---"
}