GET /api/v0.1/hansard/entries/1604284/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604284,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604284/?format=api",
    "text_counter": 239,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi nikaribishe shule hii iliyoko Mbeere South, Embu County. Karibuni sana muone yale tunatenda hapa. Tunaangalia mambo ya usalama na vile kaunti zetu zinaweza kupata pesa. Shule hii imejengwa na KenGen, lakini shule zingine za maeneo hayo zina shida. Maeneo hayo hayana maji, hospitali au chochote. Tumekuwa tukisema marupurupu ya hardship yasiondolewe. Pia, tunasema kaunti zote ziongezewe pesa ili Kaunti ya Embu iweze kutengeneza barabara, hospitali au mambo ya kilimo iendelee vizuri. Mkikaa vizuri na msikilize mambo ya walimu; mjiepushe na dawa za kulevya, miaka ijayo mtakuwa Maseneta na mengine. Ninawakaribisha. Mkirudi Nyumbani Embu, muende na salamu na pia safari njema."
}