GET /api/v0.1/hansard/entries/1604298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604298,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604298/?format=api",
    "text_counter": 253,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa fursa hii. Naunga mkono Hoja ya marekebisho iliyoletwa na Sen. Okong’o Omogeni. Ni dhahiri shahiri kwamba pesa zinapaswa kuambatana na majukumu. Majukumu mengi yamehamishwa kutoka kwa Serikali Kuu hadi kwa kaunti. Ni vigumi kwa kaunti yoyote inayopata chini ya Shilingi 6 bilioni kwa mgao wa fedha kufanya maendeleo kama kutengeneza barabara, kununua dawa katika hospitali ama kujenga shule za chekechea. Kwanza, namshukuru Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha na Bajeti, Sen. Ali Roba, kwa nia njema waliyokuwa nayo walipoandaa Hoja hii kwa kupendekeza kaunti zenye ushuru mdogo zinapaswa kuongezewa bilioni mbili. Marekebisho ya Mswada yaliyoletwa hapa siku ya leo yanapendekeza kaunti 11 ndogo ziongozewe shilingi 4 bilioni. Muhula wa Seneti iliyopita, tulifanya kazi kwa umoja na tukaweza kuongeza takribani shillingi 50 bilioni. Hata sasa sina shaka rohoni mwangu kwamba tukifanya kazi kwa umoja, tutaweza kuongeza pesa zinazoenda kwa gatuzi zetu. Kama Seneti, tulipendekeza shilingi 465 bilioni kuenda kwa kaunti zetu, lakini Bunge la Kitaifa, kwa ujuzi au ukosefu wa ujuzi, wakapendekeza shilingi 405 bilioni kuenda kwa kaunti. Hawaelewi majukumu ya gatuzi zetu. Majukumu ya kutengeneza barabara, maji na afya yamehamishwa kwa kaunti. Nilidhani wanafaa kukubaliana na sisi kwani tunajua mambo ya gatuzi zaidi. Hata hivyo, nakubaliana na pesa zilizopendekezwa na mapendekezo ya Sen. Okong’o Omogeni kuhusu fedha za usawazishaji wa kaunti. Kamati ya Fedha na Bajeti ilikuwa na nia njema kwa kupendekeza Shilingi 2 bilioni, lakini hizo ni pesa kidogo ukilinganisha na majukumu. Nakubaliana na maoni ya Sen. Eddy kwamba tuongeze Shilingi 1 bilioni ili zile kaunti zinazosemekana ni ndogo ziongezewe Shillingi 3 bilioni ili tuwe na usawa. Tukifanya hivyo, tutasaidia gatuzi zetu katika ukulima, afya, kutengeneza barabara na elimu ya chekechea. Kaunti ya Laikipia ikiwa na shida yoyote ya ukosefu wa pesa, vile vile kaunti za Nyamira, Homa Bay na Taita-Taveta zitakuwa na shida kwa sababu tumeunganika na ni kitu kimoja. Ni vizuri tutembee kwa umoja na kukubaliana ili tupate pesa hizi. Pia, hatufai kukomea kwa kupigania fedha ambazo zinaenda kwa gatuzi zetu kwa sababu utagundua kuwa pesa hizi hufujwa kwa ufisadi. Kaunti kama Nyamira ina mabunge mawili ya kujadili mambo yao. Wengine wanajadili katika sebule na wengine katika mahali panapofaa. Huo ni ufujaji wa pesa. Itakuwa ni vigumu kwa Seneta wa Kaunti ya Nyamira kutetea ongezeko la pesa, ilhali pesa zinafujwa. Kunawezaje kuwa na mabunge mawili ilhali Katiba imesema vizuri kwamba kutakuwa na bunge moja katika The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}