HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604299,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604299/?format=api",
"text_counter": 254,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kaunti ya Nyamira? Kwa hivyo, haya mambo ni mpaka yaangaliwe. Namsihi Sen. Omogeni kwa sababu ameleta Hoja hii akiwa na nia njema ya kusaidia Nyamira, lakini pesa zikifika Nyamira, zinatumiwa vibaya. Sen. Omogeni, baada ya sisi kupitisha Mswada huu, tutalivalia njuga mambo ya ufisadi na ufujaji wa pesa za umma. Vile vile, tukisema kwamba pesa zifuate majukumu, ukiangalia kama afya, pesa nyingi, zaidi ya asilimia 70 zinabaki katika Serikali ya kitaifa. Ukiangalia katika Serikali ya kitaifa, mambo ambayo wanashughulikia sana ni policy na vile vile hospitali za kitaifa ni chache. Kwa mfano, kuna Mathari Mental Hospital, Moi Teaching and Referral Hospital, Spinal Injury na Kenyatta National Hospital. Hizo tu ndizo hospitali ambazo zimebaki katika Serikali ya Kitaifa. Kwa hivyo, tukisema ya kwamba majukumu yafuatwe na pesa, tunamaanisha yale majukumu tayari yamepelekwa katika gatuzi zetu. Bi. Spika wa Muda, ingekuwa bora ikiwa tunaweza kukubaliana kwa sababu wakati huu pesa haziendi katika kaunti zetu. Tukikubaliana, tutaweza kupeleka hela katika gatuzi zetu kwa sababu Waswahili wanasema, ngoja ngoja huumiza matumbo. Ningeomba Kamati ambayo inaongozwa na Mwenyekiti wa Fedha, Sen. Ali Roba, kwamba pesa hizi ambazo tunagawana, zikipita kiwango cha Shilingi 415 bilioni, tuweze kuongeza pesa ambazo zinaenda katika hizi gatuzi ambazo zinasemekana ni ndogo tuweze kupewa Shilingi 4.6 bilioni. Wale Maseneta watakaoenda kutuwakilisha katika ile kamati ya kuleta uwiano, tupeleke Maseneta ambao wataweza kukaa ngumu. Ningeomba Seneta wa Mandera, Sen. Ali Roba, kwa sababu amekuwa akishabikia hayo mambo na ana uwezo, ujuzi na amebobea, awe mmoja wao pale ndio aweze kupeleka ujuzi pale na awaambie kinaga ubaga kisa na maana ya sisi katika Seneti kutaka pesa zaidi. Kaunti zote za Jamhuri ya Kenya zinahitaji pesa hasa hizi kaunti ndogo kama Laikipia, Nyamira, Elgeyo-Marakwet, Taita-Taveta, Kirinyaga, Embu, zinahitaji pesa ndio ziweze kujikimu na waweze kufanya majukumu waliyopewa. Leo, nataka kuunga mkono Hoja hii. Nimeketi nikasikia kuna kaunti ambazo zinapata ushuru mwingi kwa hivyo hawapati kupewa pesa zaidi. Kwa mfano, Laikipia kwa sababu sisi tunapata ushuru mwingi, hatupaswi kupewa pesa zaidi. Huwezi ukamkata mtu mkono kwa kazi nzuri aliyoifanya. Sisi tunafanya kazi nzuri ya kuweza kupata ushuru mwingi. Kwa hivyo, katika asilimia fulani, inapaswa iongezwe kwa wale ambao majukumu yao kama ni kupata ushuru, tunafanya hivyo kwa ustadi lakini sio kutukemea na kutukejeli kwa sababu tumeweza kupata pesa nyingi kutoka kwa ushuru, halafu ukifika katika Seneti, unapata Seneti hii ndio inatumia nguvu zake. Ninakurai, Mwenyekiti wa Kamati, mkirudi katika Kamati, kuangaliwe asilimia iongezwe kwa wale ambao wanafanya kazi kwa ustadi. Lakini sio kuzawadi umaskini kusema kwamba asilimia ya wale ni maskini na wamekuwa katika gatuzi hizi wapewe pesa nyingi kwa sababu ni maskini, ilhali wamekuwa katika gatuzi kwa miaka zaidi ya 12. Tunapaswa kuwatuza na kuwapa heko wale wanaofanya kazi ambayo wanapaswa kufanya. Ni wazi tunapofanya hii kazi, hawa magavana wakiitwa katika Seneti ndio waweze kuulizwa maswali, na hawaulizwi maswali kuhusu mashamba yao au boma zao, wanaulizwa maswali kuhusu pesa ambazo sisi wenyewe kama Seneti tulijadili tukatetea The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}