GET /api/v0.1/hansard/entries/1604300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604300,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604300/?format=api",
"text_counter": 255,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ndio waweze kuongezewa na kupelekewa katika kaunti zao. Wakiitwa, wanapaswa kuja na kujibu maswali. Hilo ndilo jukumu letu kikatiba; kuuliza maswali, tuweze kujibiwa ndio tuweze kuwa sisi ndio macho ya wananchi waliotuchagua katika gatuzi zetu. Magavana wengine wakiitwa wanaona wao ni kama miungu wa gatuzi walizotoka. Wanapaswa kuwajibika na kujibu maswali yale ambayo wameulizwa katika Seneti hii. Itakuwa ni kinaya kwetu sisi kuja hapa kuteta na kusema pesa zinapaswa kuongezwa, lakini baada ya wao kupata zile pesa, inakuwa sasa hawawezi kuja wakiitwa ndio waweze kuwajibika katika Seneti hii. Siku ya leo, hili ndilo jukumu letu kubwa sana kama Seneti; kulinda na kutetea gatuzi zetu. Lakini ikiwa kazi yetu itakuwa tu ni kutetea gatuzi zetu lakini baada ya wao kupata zile pesa inakuwa ni vigumu wao kuja hapa kwetu--- Inaonekana kuna nia njema. Nataka kumpongeza Mwenyekiti na Kamati yake kwa vile wamesema hawataki kaunti yoyote ibaki nyuma. Sisi sote tunapaswa kutembea pamoja. Kwa sababu ya huo upendo na hiyo nia njema, tunawapongeza. Ninaomba kamati na Bunge hili, tafadhali tupigie kura hayo marekebisho yaliyoletwa na Sen. Omogeni ndio hizi kaunti ambazo zinapata pesa kidogo ziweze kupata pesa ambazo zinaweza kukimu zile kaunti. Lakini ningependa kuwaambia Maseneta wa Embu, Kirinyaga, Elgeyo-Marakwet, Tana River na Nyamira kwamba hizi pesa tunazozitetea hapa zikiongezwa, magavana ambao hizo kaunti pesa zinaenda wanapswa kuwajibika. Hizo pesa zisitumiwe kiholela, zitumiwe kwa kazi ambayo inafaa; kazi ya kuimarisha maisha ya wananchi wa gatuzi hizo. Hizo pesa hatuwapatii ili waweze kujitajirisha wenyewe ama iwe pesa yao ya mfuko ndio mtu anatembea katika ile gatuzi, kwa mfano, Gavana wa Laikipia anatembea Rumuruti, Olmoran, Doldol, huku akipeana pesa kiholela. Hizi pesa ni za maendeleo na kuimarisha uchumi katika gatuzi ambazo tunapeleka hizo pesa. Sen. Eddy, ninakubaliana na wewe ulivyosema bilioni tatu. Lakini, hizi pesa zikitumiwa vibaya, tutakataa leo, kesho, mtondo goo na hata milele. Nikimalizia, naunga mkono marekebisho yaliyoletwa na Sen. Omogeni na vile vile yale mambo ambayo Sen. Eddy amesema, kwa sababu yeye ni mwanakamati wa Kamati ya Fedha na Bajeti. Sikudhani ana ule mwelekeo na ujuzi wa pesa vile alivyoeleza hayo maneno hapa. Ule ujuzi ambao amesema hapa, sijui kama Sen. Omogeni alimsikia. Alisema badala ya Shilingi 4 bilioni na si Shilingi 2 bilioni, akaja akasimama katikati. Nikaona ueledi alionao. Kwanza, pole kwa kumpoteza yule kijana barubaru aliyeuwawa na hawa wakora wanaosema ni maafisa wa polisi. Wameua huyo kijana na tutasimama wima kutetea haki katika Jamhuri ya Kenya. Bi. Spika wa Muda, ningependa kurudia kwa sababu hapa ndipo nina uchungu. Pesa hizi tunapeleka kwa gatuzi zetu tutazilinda kwa hali na mali na kwa uhai wetu na damu yetu. Ni uchungu tunakaa hapa, tunaongea kuhusu pesa na hatimaye, zikienda kwa gatuzi zetu, zinaingia kwa mifuko ya watu. Ningeomba Sen. Okong’o Omogeni--- Yes, I would like to be informed."
}