GET /api/v0.1/hansard/entries/1604305/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604305,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604305/?format=api",
    "text_counter": 260,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kinyua",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Bi. Spika wa Muda, hayo ni maarifa mazuri na yameniarifu kuhusu taasisi hii ambayo inapaswa kuchangamkia mambo ya ufisadi. Hii ni kwa sababu, ufisadi ndio kigezo kikubwa kinachofanya mambo yasitendeke. Kwa sababu siko kwa kamati yeyote aliyetaja na kuna taasisi inayopaswa kushugulikia haya mambo, hii taasisi inapaswa kuwajibika kabisa ndio Kenya iende mbele. Kenya itaenda mbele namna gani ikiwa gatuzi zetu zitasonga mbele? Bi. Spika wa Muda, nikimalizia, ninaunga mkono. Pia, nilitaka kueleza Sen. Okong’o Omogeni juu ya haya marekebisho. Alisema kwamba, hizi hela zimeongezwa, zisemekane ni za kazi gani, ni za kutengeneza barabara au zahanati ndio zisitumiwe kiholela. Zikifika kwa gatuzi ziwe hazina kazi. Tunafaa tuziweke ziwe na sababu fulani. Zinaenda kutengeneza mabwawa ya maji, shule za chekechea ama ni za kutengeneza barabara? Ikiwa ni barabara, ni barabara kiasi na aina gani? Nashukuru kwa kunipa fursa hii."
}