GET /api/v0.1/hansard/entries/1604314/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604314,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604314/?format=api",
    "text_counter": 269,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bi. Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi hii. Kwanza, ningependa kushukuru Kamati ya Fedha na Bajeti inayoongozwa na Mwenyekiti ambaye ni Sen. Ali Roba kutoka Mandera. Amedhihirisha tajriba na weledi wa kuongoza Kamati hiyo kwa sababu mbinu ya kugawa pesa waliopendekeza imefanya kuwe na amani hapa katika Seneti. Hata kama kuna marekebisho yatakayofanywa, ameonyesha kwamba ni kiongozi asiyejipendelea. Kwa hivyo, namshukuru kwa hilo."
}