GET /api/v0.1/hansard/entries/1604322/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604322,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604322/?format=api",
"text_counter": 277,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kitaifa. Huwa tunaenda katika Bunge la Kitaifa na kuomba. Sisi husema ya kwamba Seneti imepitisha sheria ya Division of Revenue Bill na tunataka Shilingi 465 bilioni. Tunapofika pale, huwa wanageuza na kusema ya kwamba watatupea Shilingi 405 bilioni. Sababu wanayopeana ni kwamba kuna wizi wa fedha katika kaunti zetu. Hiyo ni kweli lakini, pia kuna wizi wa pesa katika mfumo mzima wa pesa ambayo inaitwa NG-CDF. Kinachotendeka ni kwamba nyani haoni kundule. Kamati ya maridhiano inaenda kukaa chini. Lazima waende na wajifunge kibwebwe. Inafaa wajue ya kwamba watakabiliana namna gani wao wenyewe. Hii ni kwa sababu ukimwalika mbu katika kongamano la kutafuta dawa ya malaria, hakuna suluhisho ambalo atakuja nalo. Sababu ni kwamba yeye ndio jawabu ya shida ya malaria. Bunge la Kitaifa ni kama mbu ambaye amealikwa katika kongamano ya kutafuta dawa ya malaria. Hii ni kwa sababu hao ndio wamekuwa shida kubwa. Wamekuwa wakitunyima pesa za ugatuzi."
}