GET /api/v0.1/hansard/entries/1604325/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604325,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604325/?format=api",
"text_counter": 280,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kuna wengi wanasema kwamba tunafaa kuongea. Hivyo tutafanya katika kamati ya maridhiano ambayo itatengenezwa na Kiongozi wa walio Wengi Bungeni. Lakini wakati wanaenda pale, tunasitia mazungumzo ambayo yanatoka katika Bunge la Kitaifa. Ni mazungumzo ambayo hayafai. Inafika mahali ambapo hata kama kuna heshima, hata mtoto akikunja ngumi wakati mwingine inabidi agongwe kama mtu mzima kama amefikisha kiwango na amekosa heshima. Tutaenda pale, tupambane katika kamati ile na tuhakikishe kwamba tumepata pesa. Kitu ambacho hatutafanya ni kuwajibu katika mitandao wakati tunaongea mambo ya muhimi kama mambo ya hospitali na madawa kwa sababu unapopigwa teke na punda, nawe upige punda teke, nyote ni punda. Kunapaswa kuwe na tofauti kati yetu na wao, kwamba katika mitandao ya kijamii, hatutajibizana na wao lakini ile kamati ambayo tunaituma, inafaa ijifunge kimbwembwe kuhakikisha ya kwamba sisi tumepata haki yetu. Seneti hii ina akili timamu kupitisha Kshs465 bilioni. Sisi sio wanasesere kwamba hatukuwa na akili. Sisi sio vikaragosi. Kwa hivyo tunapofanya sheria kama zile na zinapofika katika Bunge la Kitaifa tunaonyeshwa madharau, ni jambo ambalo hatufai kukimya na kuacha liendelee kufanyika. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}