GET /api/v0.1/hansard/entries/1604326/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1604326,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604326/?format=api",
    "text_counter": 281,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna jambo lingine ninapomalizia. Nimeona kwa muda, wale wawakilishi wadi, katika gatuzi nyingi ikiwemo Kaunti ya Kirinyaga, wameongea na wamesisitiza ya kwamba wanataka fedha zaidi ziweze kuenda katika wadi zao. Ningependa kuwahakikishia ya kwamba sasa pesa tunaongezea. Kwa sababu ile iliyokuweko pale awali ya kwamba hamna pesa, sasa hamna. Basi tunapopitisha mfumo mpya, muendelee kupambana kuhakikisha kwamba pesa hizi zinawafikia. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo tutaweza kufanya maendeleo katika kona zote za nchi. Ningependa kumwambia Gavana pia, pesa zinapoongezwa, inafaa zimalize umaskini na kuhakikisha kwamba biashara zinaendelea kwa sababu ya kutengeneza miundo msingi na pia kupeana huduma ambazo zinafaa. Kwa hivyo pesa zile ambazo tunaokota zinafaa kuongezeka. Pesa nyingi sana ambazo zinaokotwa katika Kaunti ya Kirinyaga zinapotea. Mimi mwenyewe huwa ninazunguka ilhali wale ambao wanaokota kodi bado wanalipwa pesa kidogo. Ukienda kwa wale ambao wanahusika katika jambo ambalo linafaa kutuongezea fedha wenyewe hawaridhishwi na mishahara lakini bado pesa zinaendelea kupotea. Ni jawabu ambalo itabidi tulipate kutoka kwa Gavana wakati anapofika katika kamati tofauti tofauti. Kama ni shule za chekechea, Kaunti ya Kirinyaga yenyewe haina mpango wowote wa kupeana chakula kwa watoto wa shule za chekechea. Tunakaa na wewe katika Kamati yetu ya Elimu. Magavana wengi ambao wamekuja katika kamati ile wako na mifumo na mipango ya kupeana chakula katika shule za chekechea. Katika Kaunti ya Kirinyaga, hatuna. Pesa zinapoongezewa, ningetaka kumwambia Gavana aweke bajeti kwa sababu watoto wengi wanaumia wakati wanapoenda shule. Unapoangalia sisi watu wakubwa na ambao tuna miaka mingi; wengi wetu washakuwa wahenga hapa. Ifikapo saa nne kila siku, kuna chai tunawekewa pale pamoja na mkate, mandazi na viazi vitamu na hiyo ni baada tu ya kuchukuwa staftahi zetu katika nyumba zetu asubuhi. Je, na mtoto aliyewekwa darasani kuanzia saa moja bila kula chochote? Hilo halifai kufanyika hasa katika wakati tuliomo na katika ugatuzi ambao tayari umefanyika katika nchi yetu."
}