GET /api/v0.1/hansard/entries/1604331/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604331,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604331/?format=api",
"text_counter": 286,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Hospitali zetu hazina dawa lakini kuna mtu mwenye tumbo kubwa kama mpira na alipoajiriwa juzi alikuwa amenyooka kama mikaratusi ya Lebanoni. Wakati ameingia pale mara moja amefura kama kupe hata hajamaliza miaka miwili au mitatu. Nguo haziwatoshei. Wengine wanavaa nguo zinazoka kama marinda na ni wanaume kwa sababu ya kuzidisha. Maskini anapoamka kukimbia asubuhi kwenda kutafuta lishe, naye Mungu anafanya wakimbie asubuhi kupunguza Kisukari, Shinikizo la Damu na uzito. Hayo ndiyo mambo ya Mungu."
}