GET /api/v0.1/hansard/entries/1604335/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1604335,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1604335/?format=api",
"text_counter": 290,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Kuna sababu hata ukichukua mshipi mpya kufunga suruali iliyoraruka haitabadilisha mambo. Bado utakuwa unaonesha uchi wako. Uchi ulio katika hospitali za kaunti zetu umezidi. Unapata watu watatu wanalalia kitanda kimoja. Nguo wanazolalia ni mbaya, dawa hakuna. Hospitali kuu ya Kerugoya unaambiwa ununue dawa. Kimbimbi hakuna dawa. Hata wanaotaka kupigwa picha, huduma hiyo haiko katika hospitali zetu. Inafika watu kuuliza ugatuzi unafanya kazi gani. Magavana wenyewe ndio watafanya ugatuzi uonekana kwamba unafanya kazi."
}