GET /api/v0.1/hansard/entries/1613670/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1613670,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1613670/?format=api",
"text_counter": 89,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Munyi Mundigi",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "ambayo imeletwa na Sen. (Dr.) Murango kuhusu mambo ya maziwa. Mambo ya maziwa inashughulikiwa na Kamati ya Kilimo. Wakulima wenye wako na ng’ombe na wanauza maziwa New Kenya Co-operative Creameries (KCC) wanaumia sana. Kumekuwa na vita Kaunti ya Embu na kaunti zingine. Wananchi waliambiwa na Rais pamoja na Waziri wa Co-operatives and Micro, Small and MediumEnterprises (MSME) Development ya kwamba watauza maziwa lita moja kwa Shilingi 50. Kilio chetu ni kwamba bei ya chakula ya ng’ombe na dawa ya ng’ombe ipunguzwe ndiposa mkulima afaidike. Saa hizi, ukienda kule Mlima; Embu, Kirinyaga, Tharaka-Nithi, Meru na Nyeri, utapata ya kwamba KCC haichukui maziwa pahali ambapo inawekwa. Maziwa imekuwa nyingi. Ni huzuni sana kwa sababu wakulima wanateseka. Wale ambao walikuwa wamechukua deni wameshindwa kulipa. Wazazi wameshindwa kulipa karo na wale wagonjwa wameshindwa kupata pesa ye kuenda hospitali. Naomba tuulize waziri wa Kilimo na yule wa Co-operatives and Micro, Smalland Medium Enterprises (MSME) Development watueleze nini inaendelea. Hii ni kwa sababu Rais alisema eti maziwa haitanunuliwa chini ya Shilingi 50. Kwa hivyo, Waziri awe summoned na hii Seneti ili akuje aseme kile ambacho kinaendelea. Hii ni kwa sababu Rais alisema bei ya maziwa iende juu, lakini tunaona bei ikishuka. Katika Kamati ya Leba---"
}