GET /api/v0.1/hansard/entries/1613689/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1613689,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1613689/?format=api",
"text_counter": 108,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kinyua",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Asante Bw. Naibu Spika kwa kunipa fursa hii. Ninataka kuunga mkono taarifa iliyoletwa na Seneta wa Jimbo la Kirinyaga kuhusu ukulima wa maziwa. Ni kinaya kwa sababu, katika Jamhuri ya Kenya, Serikali imejitolea mhanga kwa kupatiana pembejeo, mbegu za kisasa na mambo mengi. Pia, wanakumbana na mambo ya kiteknolojia. Ni jambo la kuvunja moyo sana ikiwa mambo haya yatafanywa halafu shirika ambalo limepewa jukumu la kushughulikia mambo ya wakulima, haswa maziwa, hawafanyi yale ambayo yanapaswa kufanywa. Nikitembelea wakulima sehemu ya Kirinyaga, Nyeri na hata Laikipia, wale wanaotegemea mifugo, haswa ukulima wa ng’ombe kwa ajili ya maziwa, maziwa yao yote haiwezi kuchukuliwa na shirika la KCC. Vile vile, baada ya kupokelewa na Shirika la KCC, hata kulipwa inakuwa ni kizungumkuti. Vile vile, bei ambazo Serikali iliwaahidi kuwa lita ya maziwa itakuwa ikinunuliwa kwa zaidi ya Shilingi 50. Inakuwaje kila wakati ni matatizo. Tunaomba kamati inayohusika na kilimo ambayo itashughulikia jambo hili walivalie njuga na wamuite Waziri Mutahi Kagwe, aweze kueleza kwa sababu alipochaguliwa, kulisemekana yeye ni mtu aliyebobea na ana ujuzi. Sisi tunataka kuona ujuzi wake akilipa wakulima wa maziwa kwa wakati ufaao."
}