GET /api/v0.1/hansard/entries/1613983/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1613983,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1613983/?format=api",
"text_counter": 87,
"type": "speech",
"speaker_name": "Mombasa County, ODM",
"speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
"speaker": null,
"content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ninaiomba Kamati husika ishugulikie hili jambo. Haiwezekani kuwa mkulima ambaye anapanda majani chai sehemu nyingine ambayo quality yake ni same na ya kwingine, adidimizwe na anyanyaswe. Wakulima wetu lazima wapewe morali wakijua kuwa bidhaa zao zikiingia sokoni, zitachukuliwa kwa usawa. Siasa isiingizwe kwa majani, kwa sababu kama chai ya mkulima wa Kisii iko sawa na mkulima wa sehemu nyingine, mkulima wa Kisii anafaa apate usawa kwa bidhaa zake. Nikimalizia, ninampongeza dada yangu, Mhe. Dorice Donya, kwa kuleta mambo haya. Kwa sababu wakulima wengi huhangaishwa sana. Inaonekana sehemu moja ya taifa inapata uzito sana katika bidhaa wakati wengine ambao wanajibidiisha wananyimwa huo usawa. Sisi wote ni Wakenya. Wakulima wetu wote wanafaa kuchukuliwa katika mkondo mmoja ili mazao yao yaingie katika market . Utamu wa chai ni kuweka kwa maji ya moto, kuangalia uzito wake, na ikiingia kwa tumbo ni chai. Kwa hayo, ninamsifu sana dada yangu, Mhe. Dorice Donya."
}