GET /api/v0.1/hansard/entries/1614102/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1614102,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1614102/?format=api",
    "text_counter": 206,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mombasa County, ODM",
    "speaker_title": "Hon. Zamzam Mohammed",
    "speaker": null,
    "content": " Asante sana, Mhe. Spika. Ningependa kupongeza Kamati iliyowapiga msasa hawa makamishna. Wakenya walikuwa wanauliza tunaelekea wapi. Baada ya muda mrefu, wametupa jawabu kuwa ni hawa ambao wameteuliwa. Nawawapongeza makamishna wote ambao wameteuliwa, wakiongozwa na mwenyekiti wao. Wakenya tumefurahi kwa sababu tumeona kwamba wamechanganya. Leo tumepata Mwenyekiti ambaye ametoka jamii ya wachache, na hili linaonyesha kuwa Wakenya wamekubali kwamba uongozi unatoka mahali popote. Ninasimama kwa sababu ya mwanangu, ama niseme mtoto wa Pwani, Fahima, ambaye ametoka katika jamii ndogo sana pale Shela. Nilifuatilia wakati walikuwa wanapigwa msasa, na nilikuwa naangalia jinsi alivyohojiwa na lile Jopo. Niliona yule mtoto alikuwa na ujasiri mkubwa sana. Ameshika bendera ya vijana wetu na kuonyesha kuwa vijana wana nguvu na ari ya kuchukua nafasi kubwa sana katika taifa. Ningependa kuwaombea Mungu. Najua kwamba kazi hii ina mitihani mingi sana, lakini nawaombea Mungu, Insha Allah, wakati wa kuanza kazi zao walindwe na Mwenyezi Mungu. Wasimame na haki na usawa. Hatutaki kuona maafa katika taifa. Tunawategemea kutoa haki kwa wananchi. Kama Mama County wa Mombasa, ningependa kumwambia Fahima kwamba namuombea Mungu sana. Ametuheshimisha wanawake. Namuombea Mungu sana. Amefanya wanawake na vijana waheshimike. Alizungumza kwa ujasiri na kuonyesha kiwango chake cha elimu. Nimependezwa sana. Namuomba Mwenyezi Mungu ambariki pamoja na wenzake na Kenya izidi kusonga mbele. Tuko tayari kwa uchaguzi."
}