GET /api/v0.1/hansard/entries/1623611/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1623611,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1623611/?format=api",
    "text_counter": 105,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Shakila Abdalla",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante, Naibu Spika. Kesi ya Sen. Dullo imeongezeka katika list ya uhalifu unaoendelea kwa akina mama. Ni uhalifu ambao ni wa dhuluma wa kijinsia. Inafanya akina mama waogope kuingia katika siasa na kutoa maoni yao kikamilifu. Tunataka Seneti ichukue hatua kali kwa huyo Gavana. Huyo Gavana alimkashifu mheshimiwa mwenzake hadharani bila sababu. Sen. Dullo hajamkosea. Yeye alikuwa akifanya kazi wakati ambapo huyo Gavana aliitwa hapa kuulizwa maswali kuhusiana na jukumu lake la Kaunti ya Isiolo. Lakini kwa sababu anataka kuficha madhambi yake nyuma ya Mhe. Fatuma, anamdhulumu na kumkosea kwa matusi ambayo hayawezi kueleweka. Kwa hivyo, tunacondemn na kupinga dhuluma hizi za kijinsia zinazoendelea kwa akina mama, hususan wamama ambao wako katika mirengo ya kisiasa. Tunapinga na kukataa na tuamuaibisha huyo Gavana wa Kaunti ya Isiolo kwa mambo anayoyafanya. Asante."
}