GET /api/v0.1/hansard/entries/1623628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1623628,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1623628/?format=api",
    "text_counter": 122,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kibwana",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mr. Deputy Speaker, Sir, I am the former chairperson because I stepped down. Sen. Veronica Maina is the current Chairperson, ili nipatia wenginenafasi. Asante, Bw. Naibu Spika, kwa kunipa nafasi hii. Kusema kweli, jambo hili lina uchungu kwetu sisi akina mama; lina uchungu kwetu kama wanawake; lina uchungu kwa huyu gavana kumvua mwenzetu nguo. Hata mimi ninauliza, je, gavana huyu yuko na mama, dada au watoto wasichana kwake? Yeye kama kiongozi ama gavana wa jimbo alisimama na kuzungumza mambo kama hayo dhidi ya Seneta Dullo? Ninashangaa sana ni nani alimueleza kuwa Seneta Dullo anatafuta? Na kama Seneta Dullo anatafuta, kwani yeye mwenyewe hawezi kujipatia? Chochote kile alichokuwa akikizungumzia ni mambo ya kindani ya mtu mwenyewe. Ninashangaa gavana huyu alipokuwa akizungumza siku hiyo alikuwa sawa ama alikuwa ametumia mihadarati? Kusema kweli, hakuwa na akili timamu akizungumza maneno kama hayo. Sisi kama wanawake, tunashutumu vikali na tunaumia sana. Kusema kweli, vile Sen. Aaron Cheruiyot amesema, ni lazima hatua ichukuliwe dhidi ya gavana huyu. Tumeona mwenendo wa gavana huyo. Tunapomuita kwenye kamati zetu, haji. Anatoka na kuzungumza mambo mengine mabaya kuwa hawezi kuitwa na kamati. Tumeona mwenendo wa gavana huyu. Mimi ninataka kusema, ninaomba gavana huyo aweze kuangaliwa mental health yake. Hii ni kwa sababu mimi nimechampion hiyo kwa Seneti na nimesema kuwa ni lazima jambo la mental health, yaani akili taathira, ni lazima iangaliwe iwapo yuko sawa. Ninaomba akutane na madaktari ili waweze kumsaidia. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}