GET /api/v0.1/hansard/entries/1623703/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1623703,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1623703/?format=api",
"text_counter": 197,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Faki",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "kama gwiji wa sanaa. Alipigania uhuru wa nchi yetu na pia alipigana ili lugha za kiafrika ziwekwe katika map ya ulimwengu. Alitaka hizi lugha ziwe zinaweza kutumika kama lugha zingine ulimwenguni. Mtu mweupe alipokuja Afrika, alidunisha na kudharau lugha za kienyeji. Lugha nyingi hazikuwa zikitumika. Hiyo ndio sababu sisi tunatumia Kiingereza kama lugha ya kwanza ilhali tuko na lugha zetu ambazo tunaweza kutumia. Mfano mzuri ni lugha ya Kiswahili ambayo imepata matumizi makubwa katika Afrika Mashariki na Afrika ya Kati. Wakati huu, lugha hii inatumika hata kule Afrika Kusini. Lugha ya Kiswahili inatumika na inatambulika hata katika Bunge ya Afrika. Msukumo wa mwendazake Professor Ngũgĩ wa Thiong’o ulileta kutambulika kwa lugha za Kiafrika. Hiyo ilichangia katika kuunganisha Afrika. Moja ya silaha ambayo ilitumika kuunganisha Waafrika wakati wa ukoloni ilikuwa Lugha ya Kiswahili. Kwa hivyo, mchango wake ni mkubwa. Baada ya uhuru, aliona ya kwamba majina tu ndio ilibadilika na mwafrika hakupata uhuru kamili. Hii ndio sababu yake ya kukosoa muongozo ama mwelekeo ambao nchi ilikuwa inatumia ili kuendesha masuala yake. Professor Ngũgĩ wa Thiong’o alijipata pabaya kwa sababu wale ambao walikuwa mamlakani wakati ule hawakukubali fikira ambayo alikuwa nayo. Licha ya kwenda uhamisho, vitabu vyake viliendelea kusomwa. Hiyo imesaidia pakubwa kuleta mwamko wa masuala ya kiutamaduni, serikali na masomo. Hii ni kwa sababu vijana wengi wamesoma na kufuata mwelekeo wake. Juzi, wasichana walizuiliwa kuonyesha mchezo wao katika maonyesho ya sanaa ya nchi yetu. Ilikuwa ni aibu kwamba tulizuia wale wasichana ilhali hao wasichana walikuwa wakifanya vizuri kila mwaka katika masuala ya sanaa. Lazima tujiangalie upya kama taifa la Kenya. Professor Ngũgĩ wa Thiong’o amekufa ugenini kwa sababu nchi yake haikumkubali kwa sababu ya mawazo yake. Kuna watu wengi ambao wako nje. Jana, tulikuwa tukimzunguzia msichana aitwaye Rose. Huyo msichana alipelekwa mahakamani kwa sababu ya kutenabaisha watu kuhusiana na Mswada wa Fedha ambao unakuja katika Bunge la Kitaifa katika wiki inayofuata. Nchi yetu bado ina safari kubwa ya kwenda ili tuone ya kwamba ule uhuru tuliopigania unakuwa wa manufaa na kila mtu nchini ako huru kufanya vile ambavyo sheria inampasa kufanya. Ninachukua fursa hii kutuma rambirambi zangu binafsi, za familia yangu na za watu wa Mombasa kwa familia ya mwendazake Professor Ngũgĩ wa Thiong’o kwa kumpoteza mpendwa wao ambaye alikuwa kiungo kikubwa katika nchi yetu kwa masuala ya sanaa. Tunaomba roho yake ilale mahali pema peponi. Sisi ambao tumebaki katika huu ulimwengu, ni vizuri tuendeleze mafunzo na fasihi ambayo ameacha katika nchi yetu. Tunaomba roho yake ilale mahali mema peponi."
}