GET /api/v0.1/hansard/entries/1625161/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625161,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625161/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Asante sana, Bw. Spika wa muda, kwa kunipa hii nafasi ili niweze kuongea na kuunga mkono matamshi ambayo yametolewa na wenzangu siku ya leo kuhusu mchakato mzima na ombi ambao umeletwa mbele ya Seneti. Ombi hii inahusu maandishi ambayo yanaandikwa na baadhi ya magavana wanapojenga barabara, choo na vitu vingine. Ya kushangaza ni kwamba hao magavana wanapojenga makafani au mortuary kwa kimombo, huwa hawaweki picha zao. Sijui kama ni sadfa kwa wote ama ni kwa kusudi. Sio magavana peke yao ndio hufanya hivi. Tuko pia na Wabunge wa Bunge la Kitaifa. Barabara inapojengwa, ile kibao ambayo inawekwa katika ile barabara ama kitu chochote ambacho kinajengwa huwa ni kubwa na dhamani yake huwa kubwa sana kushinda fedha ambayo imetumika katika hiyo maendeleo. Ninapokuja katika Bunge la Seneti, huwa ninaona bendera za kaunti zote 47. Kila bendera iko na alama na lebo ya kaunti zote 47. Kwa hivyo, kama wanataka kutofautisha na kuonyesha maendeleo ambayo wanafanya katika kaunti zetu, ni rahisi kufanya hivyo wakitumia lebo ambazo zimepitishwa katika bunge za gatuzi. Kuna baraza la magavana na magavana wote wanafanana. Hao ni binadamu. Wengi wao wanaongea pamoja. Kwa hivyo, hatuwezi chinja bata kwa kosa la kuharisha kwa sababu bata wote huharisha. Tunachopaswa kufanya ni kutunga sheria. Tunapolaumu dobi kwa kosa la kutotakasa kamisi na weusi ni rangi yake, basi tutakuwa tunaongea na hakuna kitu ambacho tunafanya. Sisi kama Bunge la Seneti ndio tunafaa kukaa chini, kutunga sheria na kuhakikisha ya kwamba gatuzi zetu zote haziweki picha za mtu binafsi kwa sababu amefanya maendeleo ambayo anafaa kufanya. Gavana anapotumia fedha za umma na kuweka kibandiko kikubwa ambacho kinagharimu pesa nyingi kuonyesha ya kwamba amefanya kazi ni sawa na kuzawadi samaki kwa sababu ameogelea ilhali tunajua ya kwamba ni kawaida samaki kuogelea. Sisi ambao tunapitisha fedha hapa huwa tunatumia wakati wetu, tunatoa jasho na damu kupitisha zile fedha. Saa hizi, tumeng’ang’ana hata tukakuwa na kamati ya uwiano ili kuhakikisha ya kwamba magavana wamepata Shilingi 415 bilioni. Je, sisi picha zetu tutaziweka wapi ama zitabaki tu kwa mikoba kwa sababu sisi tunapitisha tu pesa na hatujapewa uwezo wa kikatiba kubandika picha zetu. Pia ningependa kusema ya kwamba sisi huongea kwa hii Seneti lakini hatusikizwi. Umuhimu wa makalio hujulikana wakati umemea jipu. Wale magavana hujua ya kwamba Seneti iko wakati wamepata shida. Tunapopitisha pesa na kuongea mambo yasiyofaa kuliko tukae chini tuvalie njuga jambo hili na kusikizana ya kwamba The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}