GET /api/v0.1/hansard/entries/1625163/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625163,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625163/?format=api",
    "text_counter": 378,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Maneno tunayoongea hapa na wakati tunaotumia tunafaa kuwa tunasikizwa. Nilisema hapo kitambo sisi ni kama mashine inayobomoa misitu ikijenga barabara baadaye inasemekana iwekwe juu ya lori isiharibu barabara na tumesema iwe hivyo. Tunafaa jambo kama hili tulizingatie and tulizungumzie. Hata kama ni kupitisha pesa kwanza tuangalie kama kuna matumizi mabaya. Siwapi magavana wosia. Mimi sio mnasimu lakini ninayoongea hapa ninajua wale walionituma hapa pia wanasema vivyo hivyo. Ukiagalia ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha, utapata ya kwamba fedha nyingi zinazopotea ni kwa mabango yanayowekwa picha. Nikiona picha ya gavana imewekwa katika bango huwa inanikumbusha kwamba katika duka unapotaka kuua mbu, utapata kuna dawa inayoitwa Doom amabayo huwa imechorwa mbu. Inaenda kuua mbu bali haina manufaa kwa mbu Haya mabango yanayowekwa na magavana katika mendeleo yanayofanyiwa mwananchi kwa pesa za umma haimaanishi kuna mambo mazuri yanayofanyika katika kaunti zetu. Gavana anapoletwa hapa kwa sababu hafuati tunayosema ashajua kwamba dunia ni gunia tofauti ni herufi moja anaanza kulia eti anaonewa na mengine."
}