GET /api/v0.1/hansard/entries/1625171/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625171,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625171/?format=api",
    "text_counter": 386,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Kuna mambo ambayo watu wanaambiwa na wengi wanapiga makofi katika kaunti zetu kwa sababu wanaona kana kwamba kazi imefanyika, lakini huwa wanachukuliwa rahisi kama bei ya chumvi. Bw. Spika wa Muda, hebu niongee kidogo kuhusu sheria ambazo zinatoka mahali kwengine ukiniruhisu kwa sababu zinaambatana. Tunafaa kuwa wangalifu wakati tunapopitisha sheria, iwe ya gavana ama yoyote ile. Ukiangalia sheria zingine saa hii, unaanza kuweweseka na nywele shingoni zinaanza kuamka. Wakati tunapopitisha sheria zinazoenda kutumika, lazima tuwe tumefanya sample. Kwa nini nasema hivyo? Sheria zinapokuja hapa ni kama msumeno. Msumeno hukata mbele na nyuma. Kwa hivyo, wakati tunapopitisha sheria, tunatia makali msumeno. Tunasahau kwamba huenda siku moja ule msumeno ukaja kukata msitu tunaojificha kama viongozi, tuachwe tukionekana uchi na kila mtu. Mwaka 2012, kuna sheria iliyopitishwa inayoitwa kwa kimombo, “Prevention of Terrorism Act (POTA)”. Sikuwa katika Bunge hili wakati huo. Kuna zingine zitaendelea kuja na kuna zingine najua nishafika hapa. Lazima tujue kwamba zile sheria tunazopitisha zitatumika inavyofaa . Leo nimetoka mahali ambapo kuna watoto 11 chini ya miaka 17 na jaji ameamua kwamba wanafaa kuachiliwa, lakini wamewekwa pamoja na watu wazima. Sheria rahisi zinazofaa kufuatwa zinatutia aibu. Unashangaa anayetuma watoto wadogo wawekwe pamoja na watu wazima, hajui kwamba kuna sheria kuhusu watoto? Ni vizuri tuwe makini tunapopitisha sheria hata kama tunasema zichungwe. Nikimalizia, kipofu anapoanza kuona, kitu cha kwanza kutupa ni ule mkongojo alioutumia kwa miaka mingi wakati alikuwa haoni. Tunapofanya kitu cha maana kama kupitisha fedha na kufikia maridhiano, wa kwanza kutemwa ni sisi Maseneta. Kwa nini tunatemwa ilhali tumepewa kila kitu? Kweli tunabweka vilivyo, lakini ni lini tutaanza kuuma? Hilo ndio swali kubwa. Kwa sababu leo tunaongelea hili, tutajadili lile. Ukienda nyumbani, utakutana tu na picha za magavana kila mahali. Nimeuliza swali hapo awali, kama maendeleo ni maendeleo, kwa sababu kuku ni kuku, jogoo ni jina, kwa nini hawaweki picha zao katika makafani, kwa kimombo, “ mortuary” ? Kwa nini hawaweki picha zao huko, wanachagua tu mahali wamejenga daraja na barabara? Barabara inapotengenezwa na kuwekwa hicho kibandiko kikubwa, ikiharibika mwaka ujao, hawaweki picha zao kwa kile kibandiko walichoweka hapo awali. Wanaweka kingine cha pili pale pale. Unaona kuna ubadhirifu na tunapoteza pesa nyingi sana. Ningeomba magavana, kama kuna ulazima wa kuweka picha zao, waweke kwao nyumbani. Huko ndio muhimu. Utendakazi wa Serikali Kuu na ugatuzi si mapenzi. Kama unataka kuweka picha, weka kwa whatsapp ama uende uzitume kwa mtu anayekupenda. Baadhi yao kweli wako na sura nzuri, lakini kuna wengine pia wako na sura nzito na wanalazimisha kuweka picha zao katika miradi ambayo hawafai kuonekana. Kuna mmoja ana sura nzito kama ule uji unaopewa wanawake wa martenity. Unapata alijenga The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Director, Hansard and AudioServices, Senate."
}