GET /api/v0.1/hansard/entries/1625427/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 1625427,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625427/?format=api",
    "text_counter": 178,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Faki",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Mhe. Spika, ningependa pia kutoa kauli yangu kuhusu Taarifa iliyoletwa Bungeni na Seneta wa Kaunti ya Kakamega. Ni kweli kwamba maandamano yaliyotokea hivi juzi yalileta hasara kubwa na maafa kwa Wakenya wengi, wengine wao wakiwa wafanyibiashara ambao hawakuhusika kabisa na maandamano hayo. Maandamano yanahabirika wakati baadhi ya watu wanalipa watu ambao wanajifanya wao ni polisi na kutembea na rungu na wanazunguka wakijaribu kuzuia maandamano. Wakati maandamo yametolewa taarifa, ni jukumu la polisi kuhakikisha kwamba sehemu ambayo maandamano yatakuwa kumewekwa usalama wa kutosha na waandamanaji wanaandamana kulingana na taarifa waliyotoa kwa polisi. Maandamano yetu yanaharibika wakati kwanza, polisi watapinga kuwepo kwa maandamao. Baadaye, wanashirikiana na majambazi wengine kujaribu kuvuruga hayo maandamamo. Hapo ndio vurugu zinatokea na watu wanapoteza mali na vijana wanapigwa risasi bila hatia yoyote. Mhe. Spika, agizo la hivi karibuni kwamba watu wapigwe risasi kwa mguu ni agizo ambalo ni hatari sana, kwa sababu hata kwenye mguu, kuna viungo muhimu ambavyo ukiviathiri mtu anaweza kupoteza maisha. Unaweza kupigwa risasi ya mguu, uvuje damu kupita kisasi na upoteze maisha yako. Kwa mfano, mwenda zake, Rex Maasai, alipigwa risasi kwa mguu na akafariki. Kwa hivyo, agizo la kupiga risasi ni hatari kwa vijana wetu. Labda, kwa baadhi ya wanaoandamana, kikubwa walichonacho ni simu zao, kwa sababu wanataka kuona"
}