GET /api/v0.1/hansard/entries/1625442/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 1625442,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/1625442/?format=api",
"text_counter": 193,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. (Dr.) Murango",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Bw. Spika, leo hii tunanoa msumeno. Tuchunge msumeno huo usije kuwa ule ambao utakata msitu ambao ndani yake tunajificha. Kuna mtu anayeogelea baharini kwa kutegemea mawimbi. Wakati mawimbi yanaposhuka akiwa hana nguo, uchi wake huonekana mchana peupe. Kwa hivyo, ni vizuri tuchunge maneno tunayosema. Naunga mkono kuwa wakora na walioharibu mali ya umma washikwe. Hata hivyo, kwa wale waliouawa pasipo sababu, familia zao zipewe ridhaa ili waendelee na maisha kwa sababu hatuwezi kurudisha uhai wao. Asante sana, Bw. Spika."
}